Historia ya Ronaldinho alivyo wa simamisha mashabiki wa Madrid Beranabeu

Ronaldinho gaucho na maajabu yake katika Elclasico alipo izima bernabeu
Ilikuwa November 19, 2005: mechi ya 12 ya La Liga msimu wa 2005/2006. Mabingwa watetezi FC Barcelona walikuwa wakiumana na Galaticos Real Madrid: Kilichotokea usiku ule kimebaki midomoni mwa wapenda soka mpaka leo.
.
Mwanzoni kabisa mwa mchezo Samuel Eto’o aliipa Barcelona uongozi na Blaugrana wakaendelea kuumiliki mchezo huku wakicheza soka safi lenye udambwi dambwi mwingi chini ya uongozi wa kichaa wa soka kutoka mjini Porto Alegre.
.
Kijana huyu alianza kuzitikisa dakika ya 59 ya mchezo; Dinho alipokea mpira kutoka kwa Deco katikati ya uwanja, akaanza kukimbia nao kwenda mbele na kumpita  Sergio Ramos na chenga hatari ya hip, akamlamba Helguera chenga ya mwili ya Samba na kisha akamtoboa Casillas.. Ronaldinho alikuwa amefunga katika moja ya siku alizocheza mpira kwa kiwango cha juu zaidi maishani mwake - katika usiku ambao alipata heshima ya kupigiwa makofi na mashabiki wa Madrid waliokuwa wamesimama uwanja mzima ‘a standing ovation’





.
“Wakati Ronaldinho alipofunga lile goli alimshangaza kila mmoja uwanjani. Nilisimama pembeni na kujiuliza mwenyewe nini kimetokea,” Samuel Eto’o alisema maneno haya baada ya mchezo.
.
Goli lake la pili lilikuja dakika ya 78 ya mchezo, na ilikuwa kama photocopy ya goli la kwanza. Alianza kukimbizana na Ramos ambaye alionekana hajiwezi mbele ya Dinho, na akiwa kwenye angle ambayo ilionekana ngumu kuweza kufanya lolote - Dinho akaachia mashine ambayo ilimpita Casillas na kuhitimisha ushindi mnono ndani ya dimba la Bernabeu. Baada ya goli hilo akaonekana shabiki mmoja mwenye skafu ya Madrid ikiinuka na kuanza kupiga makofi na baadae mashabiki wengine wakaanza kuinuka na kufanya alichokuwa anafanya - wote wakionesha kuguswa na uwezo wa kijana wa kibrazil - Ronaldo de Assis Moreira aka Ronaldinho!
:
Ronaldinho Gaucho leo amestaafu rasmi kucheza soka. Kwa hakika huyu alikuwa mchezaji fundi zaidi kuwahi kumuona akicheza soka. #KwaheriFundiGaucho

No comments