Goal technology kutua Afrika kwa mara ya kwanza ndani ya CHAN

Kwa mara ya kwanza katika soka la Afrika Teknolojia ya msaada wa video kwa waamuzi wa soka, maarufu kama VAR (Goal Technology), utaanza kutumika kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika CHAN kwa wachezaji wanaocheza  ligi  za  ndani yatakayofanyika Morocco.
Mfumo huo unaruhusu  maafisa walioko nje ya uwanja  kusaidia  waamuzi walioko ndani ya uwanja katika masuala  kama goli  linapoingia, penalti, kadi nyekundu na inapotokea mchezaji  ameadhibiwa  kwa  makosa. Mfumo  huo  umetumika  katika  ligi  ya  Italia Serie A na  Bundesliga nchini  Ujerumani.
Teknolojia  hiyo inatarajiwa  kuanza  kutumika  nchini  Morocco  wakati  michezo  hiyo  itakapofikia  robo  fainali , ambapo timu  zinazoshiriki  zinatumia  wachezaji wanaocheza  ligi  za  ndani. Timu  16  zinashiriki.

No comments