"WATU WOTE" toka kenya yajumuishwa kushindania tuzo za oscar90
Wakenya wazidi kutusua katika level nzuri kabisa baada kutenegeneza sateliti yao ya kwanza kabisa kwa Afrila mashariki pia katika tuzo za 90 za oscar awards wame ingiza filamu moja katika kinyanganyiro hicho amabapo Filamu inauhusu shambulizi la kigaidi la Alshabaab nchini Kenya ambapo watu 2 waliuawa ndani ya basi eneo la Mandera mwaka 2014.
Filamu hiyo ilikuwa imeshinda tuzo za Oscar kitengo cha wanafunzi mwaka jana na kuwa filamu ya kwanza kutoka Kenya kushinda tuzo hiyo.
Filamu hiyo ya Watu Wote imeorodheshwa kushindania kitengo cha Filamu Bora Fupi:Itashindana na filamu nyingine nne ambazo ni "Dekalb Elementary", "The Eleven O'Clock", "My Nephew Emmett" na "The Silent Child".
Filamu hiyo inayoeleza hadithi ya Kenya, kuhusu Wakenya na inashirikisha waigizaji wa Kenya, inasimulia shambulio hilo la mwaka 2014 kaskazini mwa Kenya, ambapo maudhui ya uadui wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu yanaangaziwa.
Ni mara ya kwanza ambapo filamu ya kenya imeteuliwa kuwania tuzo ya Oscars.
"Kenya sasa imepanda ngazi. Tunaongoza katika kueleza ulimwengu hadithi za Afrika," Matrid Nyaga, mwandaaji wa filamu hiyo aliambia BBC mwaka jana
Katika shambulizi hilo, Waislamu walikataa kujitenga na Wakristo walipoamriwa kufanya hivyo na magaidi wa Alshabaab kutoka Somalia.
"Ni hadithi kuhusu Kenya na undugu wa Wakenya, na inaonyesha njia mwafaka ya kukabiliana na ugaidi kote Ulimwenguni".
Filamu hiyo iliyoundwa kwa ushirikiano wa wanafunzi wa Ujerumani na watengenezaji filamu wa Kenya inalenga kuwakumbuka mashujaa wa shambulizi hilo.
Kwa miaka kadha, Kenya ilikuwa ikishambuliwa na wanamgambo wa al-Shabaab.
Mwaka 2015, wanafunzi zaidi ya 147 waliuwawa na Al-Shabab katika chuo kikuu cha Garissa kaskazini mwa Kenya.
#source BBC SWAHILI
#source BBC SWAHILI
Post a Comment