Coutinho atua Barcelona
Baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya FC Barcelona na club ya Liverpool ambao ndio wamiliki halali wa mchezaji Philippe Coutinho raia wa Brazil, leo January 6 2018 wamefikia makubaliano ya kuuziana staa huyo.
Liverpool na Barcelona zimefikia makubaliano ya kuuziana Philippe Coutinho kwa dau linalotajwa kuwa kati ya pound milioni 142 hadi 145, hivyo Barcelona wanategemea kutangaza kukamilisha usajili wa Coutinho muda wowote usiku huu wa January 6 2018.
Post a Comment