Je wajua kuwa Diamondplatnumz anakuja na WASAFI TV &RADIO stay tune!
Rais wa WCB, Diamond Platnumz ametangaza habari njema kwa watanzania hasa hasa kwa wadau wa tasnia ya habari kwamba anatarajia kufungua Wasafi FM na Wasafi TV.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Waka’ akiwa amemshirikisha msanii wa muziki wa kufoka kutoka Marekani, Rick Ross, alitoa taarifa ya ujio wa redio hiyo na TV kupitia twitter yake Disemba 30 mwaka 2017 lakini muda mfupi baadae aliifuta taarifa hiyo.
Weekend iliyopita muimbaji huyo akiwa nchini Kenya katika show za kuufungua mwaka 2018 alifanya mahojiano na kituo cha runinga cha KTN na kueleza mpango wake huo wa kufungua Wasafi FM na Wasafi TV.
Hiyo ni habari njema kwa wadau wa habari kwani kuanzisha kwa kituo hicho bila shaka kitazalisha ajira za kutosha kwa watanzania.
Post a Comment