Tevez arejea nyumbani
Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na ambaye aliwahi kuchezea vilabu mbalimbali vikubwa Duniani kama Manchester United, Manchester City na Juventus Carlos Tevez amerejea katika klabu yake ya utotoni Boca Juniors inayoshiriki ligi kuu ya Argentina mara baada ya kuondoka nchini China.
Mapema September mwaka jana aliyekua Kocha mpya wa klabu ya Shanghai Shenhua, Wu Jingui alimtupia vijembe Carlos Tevez kwa kuzidi uzito na kusema kwamba straika huyo hatojumuishwa kikosini mpaka aimarishe uimara wake.
Tevez alihamia katika ligi ya China mwezi December 2016 na kuwa mchezaji anaelipwa mshahara mkubwa kuliko wote.
Post a Comment