Swansea city baada yakuvulunda ya mwita mkombozi mpya
Klabu ya soka ya Swansea City ya nchini Uingereza imemtangaza rasmi Carlos Carvalhal kuwa ndio kocha wao mpya atakayekinoa kikosi hicho hadi mwishoni mwa msimu wa 2017/18.
Carlos Carvalhal ambaye alishawahi kuzinoa klabu za Besiktas, Sheffield Wednesday na Sporting Lisbon ataiongoza kwa mara ya kwanza Swansea dhidi ya Watford.
Taarifa rasmi kutoka kwenye mtandao wa klabu hiyo wa (www.swanseacity.com) umeeleza kuwa Kocha huyo alijiunga na Swansea jana usiku na akitokea likizoni nchini Ureno huku ikishindwa kueleza dau la usajili.
Maamuzi hayo yanakuja baada ya Desemba 21, 2017, klabu hiyo kumtimua kocha wake Paul Clement kwa kupoteza mechi 9 kwenye msimu huu katika michuano mbalimbali.
Post a Comment