Kivumbi cha January chaanza kunukia dirisha dogo la usajili
Tayari beki wa Liverpool Virgil Van Djik ameshaaga mashabiki wa klabu ya Southampton tayari kuelekea kuwatumikia majogoo wa London Liverpool kwa ajili ya msimu ujao wa EPL.
Wakati mashabiki wa Liverpool wakifurahia Van Djik kusaini Liverpool kuna habari mbaya kuhusu wao, habari mbaya ni kwamba Barcelona wametuma wawakilishi wao kwa ajili ya kukutana na Phelipe Coutinho tarehe 3 ili kuangalia namna ya kumnunua.
Ukiachana na Liverpool habari nyingine ya usajili nchini Uingereza inazihusu vilabu vya Manchester(United na City) ambao wote wanatajwa kujiandaa kutoa £50m kuishawishi Barcelona kwa ajili ya Samuel Umtiti.
Baada ya kulalamika kwamba hawajatumia sana pesa katika usajili sasa kocha wa Manchester United Jose Mourinho anajiandaa kutuma kiasi cha £60m kwa klabu ya Juventus ili kumnunua Muargentina Paulo Dyabala.
Kocha wa klabi ya Everton Sam Allatdayce ameamua kuongeza nguvu ya ushambuliaji katika kikosi chake baada ya kocha huyo kukukaribia kumnunua mshambuliaji wa Bestikas Cenk Tosun huku pia Steven Nzonzi akiwa katika rada za Big Sam.
Klabu ya Juventus imeripotiwa kukataa kiasi cha pesa £35m ambazo Arsenal wanadaiwa kutuma kwa ajili ya kutaka kumnunua mlinzi Medhi Benatia na sasa Juve wamewataka Arsenal kuongeza kiasi hicho cha pes
Post a Comment