Kim Jong-hyun toka shinee afariki duinia
Msanii kutoka kundi maarufu la muziki la Shinee kutoka Korea Kusini barani Asia, Kim Jong-hyun amefariki dunia kwa kujinyonga Jumatatu hii.
Jonghyun (27) amekutwa amefariki katika studio iliyokuwa katika nyumba za apartment zilizopo katika eneo la Gangnam mjini Seoul.
Uongozi wa SM Entertainment ambao unasimamia kundi la Shinee, umethibitisha taarifa hizo kwa kuandika, “We are sorry to share such heartbreaking and tragic news… SHINee’s Jonghyun left us suddenly.”
Baadhi ya mashabiki wa marehemu Jonghyun wakiwa katika eneo la tukio ambalo msanii huyo amejinyonga
Polisi wa Gangnam wamesema kifo cha marehemu huyo hakikuwa kinachunguzwa kama tuhuma na familia ya Jonghyun haikuomba ombi.
Polisi hao wameongeza kuwa kabla ya Jonghyun kujinyonga alimtumia ujumbe wa simu dada yake ambaye unasema, “Please let me go. Tell me I did well. Final farewell.” Tazama wimbo wa marehemu Jonghyun enzi za uhai wake.
Post a Comment