Zitto kabwe aifananisha liverpool na chama chake cha ACT wazalendo


Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo anaifananisha ile hamahama ya wanachama wa chama chake na timu anayoishabikia Liverpool FC ya nchini England.
Kama unavyojua, star wa Liverpool Philip Coutinho amekuwa akisishwa kujiunga na miamba ya Hispania FC Barcelona katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili na tayari Barca imekuwa ikituma ofa ambazo Liverpool wanazipiga chini.

Sasa leo January 4, 2018 Zitto ame-tweet ujumbe unaosomeka kwamba: “Timu yangu Liverpool imekuwa kama chama changu ACT Wazalendo. Philip Coutinho nae kasepa kaenda kujutana na Luis Suarez. Kisa? Makombe. Makombe yatakuja tu Albert Msando”-Zitto Kabwe.
Hivi karibuni kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo Nike kupitia tovuti yao ili-post picha ya jezi ya Barcelona ya msimu huu yenye jina la Coutinho picha ambayo iliambatana na ujumbe unaoashiria tayari Barcelona imekamilisha deal la kumsaini raia huyo wa Brazil.
“Phillipe Coutinho yuo tayari kuipamba Camp Now,” ujumbe huo uliandikwa kwenye tovuti ya Nike sambamba na picha ya jezi ya Barca yenye jina la Coutinho.
Baadae ujumbe huo ulifutwa baada ya mashabiki wa Liverpool kuishambulia kampuni ya Nike kwa comments kuhusiana na ujumbe walio-post kwenye tovuti yao.
Source::shaffihdauda

No comments