BRIGHT kuja na toleo lake la pili

Ata baada ya kukosolewa na mashabiki na watu maarufu kampuni kubwa ya filamu na show za Tv ya Netflix imethibitisha ujio wa toleo la pili la filamu ya BRIGHT iliyoigizwa na Will Smith na Joel Edgerton.
Rapa Chance The Rapper ni miongoni mwa watu waliokosoa filamu hii kwa kusema ‘Hapendi kuona filamu kama hizi zinaongelea ubaguzi wa rangi kwa kutumia viumbe vingine badala ya watu halisi”
Netflix wamesema walikuwa wanasubiri kuona mafanikio ya Bright Part 1 kabla ya kutangaza ujio wa Part 2, sasa wamethibitisha baada ya filamu hii kutazamwa kwa kulipia na watu zaidi ya milioni 11 kwenye tv tu katika nchi 190, bila kuhesabu waliotazama kwenye computer na simu.
Bright Part 1 imegharimu dola milioni 90
Source:;SammisagoNEWS

No comments