Ross atua chelsea je Aubemayang kutua Arsenal?

Habari kutoka mjini London zinasema tayari Ross Barkley amepasi vipimo vya afya ndani ya Chelsea, na muda wowote kuanzia sasa kiungo huyo wa zamani wa Everton anasaini mkataba wa kuitumikia Chelsea.
Klabu ya Marseille ya nchini Ufaransa inajipanga kumchukua kiungo wa Arsenal Jack Wilshere lakini pamoja na kutokuwa na namba katika kikosi cha Arsenal Wilshere haoneshi nia kuondoka Arsenal.
Tayari kiungo wa Liverpool Emre Can ameshasaini mkataba wa awali na Juventus na katika dirisha lijalo la usajili kiungo huyo atajiunga na miamba hiyo mabingwa wa nchini Italia.
Baada ya tetesi kuwa nyingi kuhusu Phellipe Coutinho kujiunga na klabu ya Barcelona, sasa klabu ya Liverpool inajipanga kutumia kiasi cha £90m kwa ajili ya kumnunua  Thomas Lemar ambaye anaonekana mbadala wa Coutinho.
Pierre Emerick Aubameyang anatajwa kama chaguo namba moja la kocha Arsene Wenger kama mshambuliaji wake Alexis Sanchez ataamua kuondoka na kwenda kujiunga na Manchester City kama inavyotajwa.
Manchester City wako tayari kutoa kiasi cha £60m ambacho kwa ajili ya kumnunua Samuel Umtiti kutoka Barcelona, mkataba wa Umtiti na Barcelona una mkataba unaomruhusu kuondoka endapo klabu yoyote itatoa kiasi hicho cha pesa.

No comments