Wenger ashikwa mbavu na FA
Chama Cha soka cha England FA kimetangaza kumfungia kocha wa club ya Arsenal ya England Arsene Wenger kwa kosa la kutoa maneno yasiokuwa ya kiungwana kwa refa Mike Dean baada ya game ya Arsenal dhidi ya West Ham United iliyomalizika kwa sare ya 1-1.
Kocha huyo raia wa Ufaransa alikuwa na hasira dhidi ya refa Mike Dean ambaye aliwapa penati ya utata West Ham United katika mchezo uliyochezwa siku ya mwaka mpya, Wenger amefungiwa kosa pia la kuingia katika chumba cha kubadilishia nguo cha refa Mike Dean.
Wenger ambaye amefungiwa mechi tatu na faini ya pound 40,000 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 120 baada ya game hiyo alitoa kauli hii ambayo inatafsirika kama kumkosea heshima muamuzi “Maamuzi haya yalikuwa ya kushangaza kidogo, mmemuona (Dean) anafanya anachotaka kitokee, baadhi ya maamuzi msimu huu yamekuwa yakifanywa dhidi yetu sio sawa”pia hiyo itakuwa ni chance moja wapo ya wenger kwenda kushuhudia mchezaji wake wa zamani George Weah aki apishwa
Post a Comment