UEFA NATIONS LEAGUE yatoa makundi
UEFA Nations League ni mashindano ya kimataifa yatakayoshirikisha mataifa ya ulaya kwa timu za soka za wakubwa. Mashindano haya yamepangwa kuanza September 2018, baada ya kumalizika kwa mashindano ya kombe la dunia - mashindano haya yataendelea mpaka June 2019. Yatachezwa kwa mfumo wa ligi na mechi zitakuwa zikichezwa katika tarehe za mechi za kirafiki za FIFA.
Makundi ya mashindano haya yamepangwa l mchana wa tarehe
Makundi ya mashindano haya yamepangwa l mchana wa tarehe
Mfumo wa upatikanaji wa washindi wa makundi ya UEFA Nations League
:
•Timu wanachama wa UEFA 55 zimegawanywa kwenye makundi manne ambayo yamepwa majina ya ‘League A, B, C, D.
:
(League A - Germany, Portugal, Belgium, Spain, France, England, Switzerland, Italy, Poland, Iceland, Croatia, Netherlands)
.
Kundi hili linaundwa na makundi 4 yenye timu 3 kila kundi.
Mshindi wa kila kundi ataingia kwenye hatua za mwisho za UEFA Nations League (semi-finals, mshindi wa 3 na final) mnamo June 2019. Nchi mwenyeji atateuliwa December 2018 miongoni mwa timu zitakazoingia fainali.
Timu 4 za chini kwenye makundi yote zitashushwa kwenye ‘League B’ kwenye mashindano ya mwaka 2020.
Timu 4 za juu kutoka kwenye kila kundi ambazo zitakuwa hazijapata nafasi ya kufuzu kwenye UEFA EURO 2020 zitaingia play offs ambazo zitachezwa March 2020.
:
(League B - Austria, Wales, Russia, Slovakia, Sweden, Ukraine, Republic of Ireland, Bosnia and Herzegovina, Northern Ireland, Denmark, Czech Republic, Turkey)
:
Timu zitagawanywa kwenye kwenye makundi madogo 4 kila kundi likiwa na timu 3. Washindi wa makundi watapandishwa kwenye ‘League A’ - timu 4 zitakazomaliza chini zitashushwa kwenye ‘League C’ kwenye mashindano yatakayofuatia mwaka 2020.
Timu 4 za juu kutoka kila kundi ambazo zitakuwa hazijafuzu kwenye UEFA EURO 2020 zitapata nafasi ya kucheza play off March 2020.
:
(League C - Hungary, Romania, Scotland, Slovenia, Greece, Serbia, Albania, Norway, Montenegro, Israel, Bulgaria, Finland, Cyprus, Estonia, Lithuania)
.
Timu zitagawanywa kwenye makundi kwenye 4 yenye timu 3 kwenye kundi 1, na makundi 3 mengine yenye timu 4 kila kundi. Washindi kutoka kila kundi watapanda daraja kwenda ‘League B, na timu 4 za chini kushushwa ‘League D’ kwenye mashindano ya 2020.
Timu 4 za juu kutoka kila kundi ambazo zitakuwa hazijafuzu kwenye UEFA EURO 2020 zitapata nafasi ya kucheza play off March 2020.
League D - Azerbaijan, FYR Macedonia, Belarus, Georgia, Armenia, Latvia, Faroe Islands, Luxembourg, Kazakhstan, Moldova, Liechtenstein, Malta, Andorra, Kosovo, San Marino, Gibraltar
.
Timu zitagawanywa kwenye makundi 4 kila kundi likiwa na timu 4, huku washindi wa kutoka kila wakipanda daraja kwenda League C kwa mashindano ya 2020.
Timu 4 za juu kutoka kila kundi ambazo zitakuwa hazijafuzu kwenye UEFA EURO 2020 zitapata nafasi ya kucheza play off March 2020.
##source:shaffidauda:instagram account
Post a Comment