Kunakitu hukijui kuhusy Lupita Nyong'o katika movie iliyo mpa tuzo ya Oscar nakujuza hapa
Je wajua kuwa mavazi pichani aliyovaa Lupita Nyong'o(34) katika filamu yake ya kwanza Hollywood iliyompa tuzo ya Oscar, 12 Years A Slave(2013) ni mavazi halisi ya watumwa ambayo yalivaliwa na watumwa halisi katika story hiyo ya kweli miaka ya 1850s
.
Costume designer wa movie hiyo iliyoshinda filamu bora mwaka 2014 kwenye Oscars, Norris amesema mavazi ya waigizaji wengine walifanya research kubwa na kuyatengeneza kwa mkono materials walipata London na viatu waliagiza kutoka Italy. Lakini mavazi ya Lupita aliyovaa yalikuwa halisi ya wakati husika baada ya kuhifadhiwa. Costume designer huyo ni nominee mara 5 wa tuzo za Oscars kwa miaka tofauti .
Katika kujiandaa na uhusika wake Lupita alifanya utafiti mkubwa wa uhusika wake ikiwemo kusoma kitabu husika cha story ya movie hiyo, Kisha Lupita kwa utafiti zaidi alienda katika jumba la makumbusho la Blacks In a Wax huko Baltimore ambapo kuna maelezo ya kina kuhuhu Patsey aliyemuigiza kwenye movie hiyo
.
Lupita pia amesema haikuwa rahisi kupata nafasi hiyo kwasababu alifanya auditions za masaa kadhaa kwa siku tofauti kwanza casting director alimfanyia auditions alipompitisha akamwambia tena kuwa bado kuna audition ya director wa movie husika yaani Steve McQueen ambaye pia alimfanyia Lupita usaili kwa masaa kadhaa siku tofauti kutoka kwa waigizaji wengine waliokuwa wakiwania nafasi hiyo
.
12 Years A Slave ilitengenezwa kwa bajeti ya $17.1 million sawa na billion 38.37 za Kitanzania Lakini kwenye majumba ya cinema ikaingiza $187.7 million zaidi ya billion 421.23 za Kitanzania.
Source:Instagram
Post a Comment