Mfalme wa jazz Hugh Masekela Amefariki usiku wakuamkia leo
Miongoni mwa malegendary wa muziki wa Jazz Afrika Hug Masekela alizaliwa April 4,1939 nchini Afrika Kusini ni mashuhuri katika upulizaji wa tarumbeta katika muziki wa Jazz, anafahamika ulimwenguni kote kwa aina yake ya muziki anaoufanya ambao ni wa kipekee na ukilinganisha na wanamuziki wengine wa Jazz.
Hugh Masekela alifanya ziara nchini Marekani ambapo pia alifanya mafunzo yake ya muziki huko ikiwemo na Uingereza mpaka kufikia Agosti 2000 Hugh Masekela alikuwa ameuza nakala milioni 50 na kumfanya apate tuzo ya Platinum.
Hugh Masekela ameshirikiana na wasanii mbalimbali enzi za uhai wake kama Miriam Makeba wa Afrika Kusini na Paul Simon wa Marekani.
Hugh Masekela amefariki leo January 23,2018 akiwa Johanesburg, Afrika Kusini, baada ya kusumbuliwa na kansa ya tezi dume kwa muda mrefu amefariki akiwa na umri wa miaka 78.
Post a Comment