Drogba aludisha fadhila zake Ivory cost kwakujenga shule

Mwanasoka Didier Drogba, mwenye asilia ya Ivory Coast, amefungua shule ya kwanza ya msingi , na kutangazwa leo.
Shule hiyo inatarajiwa kuwasaidia maelfu ya watoto walioko vijijini kwenye mashamba ya kakao ya jamii jamii ya Pokou-Kouamekro kupata elimu bora imearifiwa.
Katika sherehe za ufunguzi wa shule hiyo, Drogba alisema, tumeshughulika na mradi huu kwa miaka miwili na ninayo fahari kuona umekamilika.
Imani ya shirika langu daima imekuwa mara zote watoto wakipata fursa ya kupata elimu bora na huduma za afya zilizo bora, tutajenga kizazi chenye madaktari, wanasayansi, wafanya biashara wa kiume na wa kike na ndivyo tutakavyo ijenga Afrika iliyo bora zaidi.
Shule hiyo imejengwa chini ya ufadhili wa shirika la Didier Drogba, kwa ushirikiano mkubwa na kampuni ya Nestlé na mpango wa kimataifa wa uimarishaji zao la kakao .
Shule hiyo ina idadi ya vyumba vya madarasa sita, darasa la awali, kantini , maliwato, uwanja wa soka na nyumba za waalimu watatu.

No comments