Watoto wa jangwani wa tamba FA
Klabu ya Yanga imeendelea kusonga mbele kuwania kulibeba Kombe la Shirikisho ASFC baada ya kuitwanga klabu ya Reha kwa mabao 2-0 na kuendelea hatua ya tatu ya mtoano ya kombe hilo.
Reha ilionyesha soka safi katika mechi hiyo iliyocheza kwenye UWanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, hadi dakika ya 80 bado ilikuwa 0-0.
Kunako dakika ya 82 Pius Buswita alifungua akaunti ya magoli kabla ya Amis Tambwe kufunga akaunti hiyo dakika mbili baada ya goli la kwanza.
Reha walio daraja la pili walijitahidi kuonyesha soka safi na kuzua hofu kwa mashabiki wa Yanga kwa kuwa walikuwa wana kumbukumbu ya kile kilichowatokea watani wao Simba ambao wamevuliwa ubingwa na Green Worriers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili pia.
Hata hivyo mbio za klabu ya Reha kufukizia kombe hilo zilikosa matumaini baada ya Tambwe kitu ambacho kiliwafanya kukosa ari na mpaka mwisho wa mchezo, Yanga SC 2-0 Reha FC.
Post a Comment