Wizkid & Davido watoa somo kwa mahasimu wa muziki Tanzania
Wasanii wakubwa nchini Nigeria Wizkid na Davido usiku wa kuamkia leo Desemba 25, 2017, wamewaacha midomo wazi mashabiki wao ambao tangu mwaka 2013 walikuwa wakiamini kuwa wawili hao wanatofauti kama sio bifu katika muziki.
Wizkid na Davido wakitumbuiza jukwaani
Wawili hao jana Desemba 24, 2017, kwenye tamasha la Wizkid The Concert lililoandaliwa na Wizkid, Davido alipanda jukwaani na kutumbuiza pamoja na Wizkid.
Surprise hiyo iliamsha shangwe kwa mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha hilo na kuondoa tetesi za muda mrefu kuwa wawili hao wana bifu.
Nzuri zaidi ni kwamba hata wimbo ulioimbwa haukuwa wa WizKid bali ulikuwa ni wimbo mpya wa FIA wa Davido.
Hii ni mara ya kwanza kwa mastaa hao kutumbuiza kwa pamoja nchini Nigeria Tangu mwaka 2015 walivyotumbuiza kwa pamoja.
Soma zaidi – Video: Davido na Wizkid watumbuiza pamoja kwenye jukwaa moja Lagos
Hii inatoa picha ya moja kwa moja kuwa ni funzo tosha kwa wasanii wakubwa hapa Tanzania, Diamond Platnumz na Alikiba kuwa ni muda wao kuwashangaza mashabiki wao ambao kila siku wanapandikiza chuki za kukuza bifu kati ya wawili hao.
Je, ipo siku tutashuhudia Diamond akitumbuiza jukwaa moja na Alikiba kwenye show maalumu ya Diamond au Alikiba kutumbuiza kwenye ya Diamond? Acha tusubiri muda utatuambia.
Tukio hilo la Davido kumpa sapoti Wizkid limepokelewa kwa mtazamo chanya kwa mashabiki wao duniani kote na wapenzi wa muziki nchini Nigeria. Soma baadhi ya maoni ya mashabiki na video ya tukio hilo
Source: Bongo5.com
Post a Comment