Mchezaji bora kuamuliwa na mashabiki wa mpila
Rais wa shirikisho la soka barani Afrika Ahmad Ahmad wakati anaingia madarakani aliahifi mabadiliko kiutendaji lakini pia katika maeneo mengine ya ambayo yanagusa mambo ya kiufundi kama mashindano na mambo mengine ambayo yapo chini ya shirikisho hilo.
Miongoni mwa mabadiliko ambayo Ahmad Ahmad aligusia ni namna ya kumpata mchezaji bora wa Afrika, January 4, 2018 mchezaji bora wa Afrika atachaguliwa. Mfumo uliozoeleka awali ilikuwa ni kwamba, makocha na manahodha wa timu za taifa ndio walikuwa na jukumu la kuchagua (kupiga kura) kwa ajili ya mchezaji bora wa bara la Afrika.
Kwa sasa shirikisho la soka Afrika limeongeza kipengele kingine cha kumpata mchezaji bora wa Afrika, ukiacha makocha pamoja na manahodha wa timu za taifa, wadau kwa maana ya mashabiki, watakuwa na fursa ya kuchagua mchezaji bora wa bara la Afrika.
Ni mabadiliko mengine ambayo tunayashuhudia chini ya Ahmad Ahmad kutokana na sera yake wakati anaingia madarakani kwamba mabadiliko ni lazima kwa shirikisho la soka Afrika.
Wachezaji ambao wameingia fainali kuwania tuzo ya mchezaji bora Afrika ni Mohamed Salah, Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang
Post a Comment