Je wajua mtaa wa Anfield(machinjioni) na Mfransa Thier Henry ndo vitu peke vilivyo kuwa vinamtisha John Terry
“Unaweza ukawa uko hotelini na ukawa unajisikia vizuri tu lakini nikitoka tu hotelini woga ulianza kunijia” hivyo ndivyo John Terry anavyoanza kuelezea safari kuelekea Anfield kuwakabili Liverpool.
Terry anasema Anfield haikuwa sehemu nzuri kwake wakati akiwa Chelsea kwani mashabiki wa Liverpool walikuwa wanashangilia sana, na mbaya zaidi walikuwa wakianza kushangilua mtaani katika barabara za kuelekea uwanjani.
Terry amekiri kwamba barabara za kuelekea Anfield huwa zinaogopesha wakati wa mechi kwani kabla hata hujaingia uwanjani unaweza kuanza kuhisi nini unakwenda kukutana nacho uwanjani kabla hata hujafika na hiyo ndio ilikuwa timu ngumu Terry aliyoihofia.
Sasa achana na Liverpool, John Terry alikuwa hapendi hata kidogo kuiona jezi ya Thiery Henry, Terry anakiri kwamba Henry alikuwa mshambuliaji ambaye alikuwa akimpasua sana kichwa uwanjani.
Siku moja kabla ya kuikabili Arsenal Terry alikuwa halali vizuri akimuwaza Thiery Henry na kila wakati alikuwa akihofia kucheza dhidi yake, baada ya kuondoka Chelsea kwa sasa John Terry anakipiga katika klabu ya Aston Villa.
SOURCE;shaffihdauda.com
Post a Comment