PAKA TIBS NA BLACKIE WAANZILISHI WA AJILA ZA PAKA

Nadhani utakuwa unamjua mnyama anayeitwa paka, ni kiumbe kinacho fugwa na binadamu sana sana kwa ajili ya ulinzi na panya ambao huwa ni wahalibifu wa vitu vya nyumbani na watu wengine hupenda kufuga paka kwa ajili ya shida zao binafsi sana sana wa zungu kwani nikumbe kinacho vutia sana hasa pale utakapo kifuga na wengine hukiuza kiumbe hicho,
Image result for cat

Mnamo mwaka 1868 paka wawili waliajiriwa rasmi kamawawindaji wa panya katika ofisi ya huduma ya kuagiza na kutuma pesa mjini London.
Walilipwa mshahara wa shilingi moja kwa wiki, pesa ambazo zilikwenda kwa wamiliki wao - na walipewa miezi sita ya kipindi cha kuchunguzwa ikiwa kweli wanaimudu kazi hiyo.
Bila shaka walitekeleza majukumu yao ipasavyo kwani mwaka 1873 walitunukiwa kwa nyongeza ya mshahara.
Paka TibsMatumizi rasmi ya paka kwa kazi za ofisini yalienea katika ofisi nyingine.
Kwa mujibu wa makavazi ya posta, paka maarufu alikuwa alikuwa ni Tibs.
              
Alizaliwa Novemba 1950, akiwa na uzito wa kilo 10.4 na kuishi katika kwenye klabu ya vinywaji ya makao makuu ya posta iliyopo kati kati mwa jiji la London.
Paka wa mwisho wa makao makuu ya Posta London alikuwa ni , Blackie,aliyekufa Juni 1984, na tangu wakati huo hakuna paka aliyewahi kuajiliwa pale
Mamlaka za Ubelgiji haziwezi kusahaulika kwani miaka ya 1870s ziliwaajiri paka 37 kuwasilisha mizigo kwa njia ya mifuko isiyowea kuingiliwa na maji ambayo ilifungwa kwenye kola za mashati yao.
Lilikuwa ni wazo lililotolewa na jamii ya wabelgiji kwa lengo la kuwatumia paka wa nyumbani , ambapo walidhani paka hawapewi mwongozo ipasavyo
 Na hao ndo paka je wewe unamtumiaje pak?


No comments