Mjengo wa trump wa waka moto
Maafisa wa kuzima moto wameitwa katika jumba la Trump Tower katika kisiwa cha Manhattan jijini New York kuzima moto uliokuwa umezuka kwenye ghorofa ya juu ya jengo hilo.
Idara ya kuzima moto ya New York imesema moto huo ulidhibitiwa na kwamba hakukuwa na majeruhi.
Shirika la habari la CBS News limesema moto huo ulizuka mwendo wa saa moja asubuhi saa za huko (saa sita mchana GMT) karibu na paa la jumba hilo la ghorofa 68.
Jumba hilo lilikuwa makazi rasmi ya Bw Trump kabla ya kuapishwa kwake karibu mwaka mmoja uliopita.
CBS News wamepakia picha za wazima moto wakiwa kwenye paa la jumba hilo huku moshi ukifuka kutoka kwa sehemu moja ya jumba hilo.
SOURCE: BBC SWAHILI
Post a Comment