Lukaku kuisihitaki Everton kwa sakata la uchawi

Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku anazungumza na mawakili wake kuhusu madai yaliotolewa na mmiliki wa Everton Farhad Moshiri kwamba aliamua kuondoka katika klabu hiyo baada ya kupata ''ujumbe wa uchawi''.
Moshiri aliuambia mkutano wa wamiliki wa hisa katika klabu hiyo kwamba Lukaku mwenye umri wa miaka 24 alipokea ujumbe huo baada ya kuzuru Afrika.
Lukaku alijiunga na United kwa pauni milioni 75 mwezi Julai baada ya kukataa kandarasi mpya Everton.
Mwakilishi wa mchezaji huyo aiambia BBC michezo kwamba uamuzi wa Lukaku haukushinikizwa na uchawi.
Msemaji huyo aliongezea: Hapendi kufuata imani kama hizo na sasa anatathmini hatua za kisheria anazoweza kuchukua.
BBC michezo inaelewa kwamba raia huyo wa Ubelgiji amekasirishwa na madai hayo.
Wawakilishi wake wanasema kuwa Lukaku alikataa kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi katika historia ya klabu ya Everton ili kuweza kucheza katika klabu kubwa duniani.
Wawakilishi wake waliongezea: Romelu ni mfuasi wa kanisa katoliki na kwamba haamini uchawi. Hakuwa na imani na Everton mbali na mradi wa bwana Moshiri.
Hiyo ndio sababu hakutaka kutia kandarasi nyengine.

No comments