Griezman aisababishia Barcelona kesi........
Club ya Atletico Madrid imetangaza kuwa itaishitaki club ya FC Barcelona ya Hispania kwa shirikisho la soka duniani FIFA kwa madai kuwa wamemfuata kumshawishi mchezaji wao Antoine Griezmann kujiunga na timu yao kinyume na taratibu.
Atletico Madrid wanaamini kuwa mazungumzo ya kinyume na sheria kati ya FC Barcelona na Antoine Griezmann yamefanyika, kitu ambacho hawawezi kukifumbia macho na watalifikisha suala hilo katika ngazi za juu za shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.
Post a Comment