Delima aipiga chini Barcelonabna atoa sababu zake
Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama FC Barcelona na Real Madrid Ronaldo de Lima jina lake limechukua headlines baada ya kufanya mahojiano na kuulizwa kati ya Real Madrid na Barcelona anaipenda timu gani?
Swali hilo lilikuja kutokana na staa huyo amewahi kuvichezea vilabu vyote, kuanzia mwaka 1996-1997 aliichezea FC Barcelona kabla ya kujiunga na Inter Milan ya Italia na baadae 2002-2007 akaanza kuichezea Real Madrid, hivyo amefunguka na kueleza anaipenda Real Madrid na akataja sababu.
Ronaldo amekiri kuipenda Real Madrid sio tu kutokana na kuichezea muda mrefu lakini anaamini Barcelona ni timu ambayo ilikuwa haitaki kuwasaidia wachezaji wake kutokea Brazil washinde Ballon d’Or, kingine amesema Barcelona wachezaji wengi huwa hawaondoki vizuri ukianzia yeye, Ronaldinho, Romario na hata Neymar.
Post a Comment