KUelekea 2018 tetesi za usajili hizi hapa

Manchester City inakaribia kumsajili kwa dau la £60m beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Telegraph)
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho analenga kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Paulo Dybala, 24, katika dau la £60m kutoka Juventus. (Daily Star)
Wakati huohuo manchester United imeimarisha dau lake kwa kiungo wa kati Marouane Fellaini, ili kumzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 ambaye I yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu (Daily Express)

Maroune Fellaini
Image captionMaroune Fellaini

United pia imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa Bordeaux ,20, Malcom, huku mkufunzi Jose Mourinho akiajindaa ku;ipa dau la £33m. (Daily Mail)
Arsenal wameambia kwamba ni lazima walipe dau la £40m kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Julian Draxler, 24, kutoka Paris St-Germain. (Mirror)

Arsenal wameambia kwamba ni lazima walipe dau la £40m kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Julian Draxler, 24, kutoka Paris St-Germain. (Mirror)
Image captionArsenal wameambia kwamba ni lazima walipe dau la £40m kumsajili mshambuliaji wa Ujerumani Julian Draxler, 24, kutoka Paris St-Germain. (Mirror)

The Gunners wako katika ushindani mkali na Liverpool wa kutaka kumsajili mshambuliaji wa PSV Eindhoven Hirving Lozano mwenye umri wa miaka 22, ambaye ana thamani ya £42m. (Daily Star)
Hatahivyo usajili wa mchezaji huyo wa hadi £35m utaifanya Arsenal kumuuza mshambuliaji wake Alexis Sanchez, 29, mnamo mwezi Januari. (Daily Mail)

Antonio Conte aomba kusajili wachezaji watatu zaidi
Image captionAntonio Conte aomba kusajili wachezaji watatu zaidi

Mkufunzi Antonio Conte ameitaka usimamizi wa Chelsea kuwasajili wachezaji watatu wapya mnamo mwezi Januari. (Mirror)
Mkufunzi mpya wa West Ham David Moyes ana hamu ya kumsajili Steven Nzonzi iwapo Sevilla itaamua kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 mwaka ujao. (Guardian)

Moussa Dembele
Image captionMoussa Dembele

Celtic Imekana madai kwamba imekubali ombi la £18m kumuuza mshambuliaji Moussa Dembele, 21, kutoka . (Sun)
Mkufunzi Roy Hodgson anahofia kwamba Crystal Palace italazimika kumuuza Wilfried Zaha mwezi ujao huku Manchester City, Chelsea na Tottenham zote zikimtaka winga huyo ,25, (mirror)

Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha kuuzwa
Image captionWinga wa Crystal Palace Wilfried Zaha kuuzwa

Uingereza inatarajiwa kucheza mechi ya kujiandaa katika uwanja wa Leeds huku meneja Gareth Southgate akataka kuungwa mkono kabla ya michunao ya kombe la dunia ya 2018 nchini Urusi.(Times, subscription required)
Mkufunzi wa Everton Sam Allardyce amefichua kwamba aliisaidia kuimarisha motisha ya mabeki Michael Keane na Ashley Williams kupitia usaidizi wa mchezo wa runinga wa The Cube. (Liverpool Echo)

No comments