Simba chali mapinduzi kichuya agoma kuludi benchi la ufundi

Baada ya klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba kupoteza mchezo wao dhidi ya Azam FC kwa goli 1-0 juzi, leo Jumatatu ya January 8 2018 walikuwa wanatupa karata yao ya mwisho dhidi ya URA ya Uganda lakini huo ukiwa ni mchezo ambao utaamua hatma ya Simba SC.
Simba walikuwa nafasi ya tatu wakiwa na point nne, Azam FC wakiongoza Kundi kwa kuwa na point 9 wakifuatiwa na URA waliokuwa na point saba, hivyo ni wazi mchezo wa leo wa URA dhidi ya Simba SC ulikuwa kama ni fainali kwa timu hizo kwani Simba alihitaji ushindi ili afuzu kucheza nusu fainali huku URA akihitaji sare.
Bahati haikuwa kwa Simba na dakika ya 48 Kalama Debossi akapachika goli la ushindi kwa URA lililodumu kwa dakika zote 90 na kufanya ubao wa matokeo usomeke 1-0, nyota wa Simba Shiza Kichuya aligoma kukaa kwenya benchi la timu yao baada ya kocha kumtoa dakika ya 53 na kuingia MO Ibrahim.

No comments