Yaliyo mkuta Emanuel Eboue nifundisho
Moja kati ya habari kubwa zinazochukua headlines kwa sasa katika upande wa michezo ni kuhusiana na stori ya staa wa soka wa kimataifa wa Ivory Coast aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali Ulaya kama Arsenal na Galatasaray ya Uturuki Emmanuel Eboue.
Eboue kwa sasa ana umri wa miaka 34 na anaitumikia adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja na FIFA kwa kushindwa kumlipa wakala wake, Eboue licha ya kutokea katika maisha magumu Ivory Coast alifanikiwa kutengeneza pesa nyingi akiwa katika Ligi Kuu England akiitumikia Arsenal kwa miaka saba.
Beki huyo wa zamani wa Arsenal kwa sasa yupo katika maisha magumu na analala chini kwa rafiki yake huku akishindwa kulipia pesa nguo zake ziende dry cleaner, hivyo analazimika kufua kwa mikono, Eboueanatajwa kuelekea kufilisika kutokana na kutalakiana na mkewe.
Hivyo kinachopelekea Eboue kuwa masikini ni kutokana na utajiri wake wote kumuandikisha mkewe, kisheria wakiachana mali zote zitakuwa za mwanamke ambaye amezaa nae watoto watatu, kwa sasa Eboue nyumba anayoishi London mkewe ambaye wameachana anakaribia kuiuza.
Jambo ambalo Eboue linamfanya aumie kichwa na kuweka wazi kuwa mara kadhaa linamjia wazo la kujiua kichwani kwake na anaomba Mungu aliepuke, Eboue ameichezea Arsenal kwa miaka saba kabla ya mwaka 2011 kuamua kujiunga na Galatasaray ya Uturuki.
“Pesa zote ambazo nilikuwa naingiza nilikuwa natuma kwa mke wangu kwa ajili ya watoto wetu, nikiwa Galatasaray Uturuki nilikuwa naingiza euro milioni nane na nilikuwa namtumia euro milioni 7, chochote alichokuwa anataka nisaini nilikuwa nasaini”>>>Eboue
Post a Comment